Mke wa Rais Mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete ameungana na Wanawake Viongozi mbalimbali kutoka Afrika katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake Viongozi unaofanyika nchini Burundi kuanzia tarehe 24-26 Octoba 2019
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) anashiriki Mkutano huo wa siku 3,ambao umeanza Oktoba 24 na kufunguliwa na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
Mkutano huu umehudhuriwa na Mke wa Rais wa Burundi mwenyeji muandaaji Mama Denise NKURUNZIZA, Naibu Rais wa pili wa Bunge la nchi hiyo, Jocky Chantal NKURUNZIZA, na Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini Burundi, Dr. Edmud Juma Kitokezi.
Viongozi wengine ambao wamehudhuria Mkutano huo ni pamoja na Naibu Karibu Mkuu UN anayeshughulikia maswala ya Afrika Mama Bintou Keita , Mke wa Rais wa Congo Brazaville Mama Antoinette Sassau Nguess,Mke wa Rais wa Central Africa Republic Madam Brigette Touadera.