Ajali si kitu cha kuzoeleka, lakini ni rahisi sana kuepuka ajali barabarani kwa kuzingatia
sheria na kanuni za barabarani, mara nyingi ajali nyingi husababishwa na uzembe
mdogo mdogo unaofanywa na madereva ambao hujiona ni madereva bora kuliko
dereva mwingine yeyote aliyopo barabarani.
Madereva wengi wenye uzoefu wa kuendesha barabarani hujikuta wakijiamini kupita
kiasi huku madereva ambao bado si wazoefu barabarani hujikuta kuwa makini haswa,
jambo ambalo ni zuri na muhimu kuzingatiwa na dereva yeyote aliyopo barabarani
kwani.
Kupokea simu, kuchat kwa njia ya meseji, kusinzia au kuendesha gari ukiwa umelewa
ni mambo ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele sana kwani yamekuwa kwa kiasi
kikubwa yakisabisha ajali mbalimbali barabarani hata kanuni na sheria za usalama
barabarani imekuwa ikikemea vikali sana tabia hizo na kusisitiza zaidi madereva
kufuata kanuni za barabarani lengo likiwa ni kuepusha ajali zaidi.
Hapa chini nimekuwekea mambo makubwa na ya msingi 9 ambayo yanaweza
kukusaidia na kukufanya kuwa dereva mzuri unapokuwa barabarani.
- Angalia Mbele: Hapa tunazungumzia madereva waopenda kuendesha gari huku
wakiwa wanatumia sim au kugeuka geuka nyuma au maongezi na abiria wako. Mambo
hayo na yanayofanana na hayo yanaweza kumtoa dereva kwenye utulivu wa barabara
na hivyo inapotokea dharula kama watumiaji wengine kukatiza ghafra mbele yake
huweza kusababisha ajali. - Usiisogelee sana gari ya mbele yako. Zaidi tunaongelea gari inapokua kwenye
mwendo, ambapo imekua jambo la kawaida kwa madereva wengine kuwasogolea sana
wenzao bila kujali dharula inayoweza kumpata huyo wa mbele kama kufunga break za
ghafra au kupasukiwa tairi jambo linaloweza kusababisha ajali hiyo ikukumbe na wewe
kwa kua uwezekano wa kukimudu chombo ukiwa kwenye mwendo na karibu zaidi ya
mwenzio wa mbele ni mdogo. - Epuka Break za ghafra. Matumizi ya break za ghafra iwe ni chaguo la mwisho, lakini
muhimu ni kuhakikisha unakadiria barabara yako na hivyo ushike break taratibu. Iwapo
utashika kwa ghafra huku gari ya nyuma yako ikiwa imekufata kwa karibu kuna
uwezekano wa kutokea ajali. Mara nyingi hili linatokea kwa madereva wanapoamua
ghafra kusimama kwenye zebra ili watembea kwa miguu. - Gia ya Manual. Watanzania walio wengi tunaotumia gari binafsi hatufahamu namna
ya kutumia gari zenye gia ya manual, badala yake tumezoea Automatic, lakini dereva
mzuri ni yule anayejifunza kutumia gia za aina zote yaani Manual na Automatic kwa kua
faida ya Manual ni kua inachangia kwenye matumizi madogo ya mafuta, lakini pia
humuongezea dereva ujuzi zaidi awapo barabarani kwa kua kila kitu anakifanya yeye
mwenyewe manually. Zaidi wakati wa dharula dereva hatohitaji aje dereva mwingine
kutoka mbali aendeshe hilo gari manual bali yeye mwenyewe ataingia na kuendesha
gari hilo. - Usikae upande uwapo kwenye usukani. Baadhi ya madereva hukaa upande kwenye
magari yao jambo linalowafanya kujisahau na kukanyaga mafuta badala ya break au
break badala ya mafuta au mda mwingine kujikuta akikanyaga vyote kwa pamoja hali
inauoweza kusababisha ajali. Na kwa safari ndefu mkao wa upande utamfanya dereva
ahisi maumivu ya mgongo au kiuno. Inaushiliwa kukaa kwa kunyooka kwenye usukani
na kurelax mwili huku ukiwa makini na watumiaji wengine wa barabara. - Kurudi nyuma. Hili ni tatizo kubwa kwa akina mama wengi na baadhi ya wababa pia.
Ni muhimu kujifunza kwa kufanya mazoezi ya kurudisha gari yako nyuma bila kuhitaji
msaada kwa kua kuna siku utahitaji msaada utakosa na hivyo unaweza kuligonga gari
lako kwa kushindwa kufanya makadirio mazuri kwa kutumia vioo vyako ya pembeni na
ndani, unapoona unashindwa kabisa kutumia vioo basi geuza shingo ili kuweza kufanya
hayo makadirio na kuona vizuri nyuma. - Kuegesha gari. Kwa sasa kwenye miji mikubwa kuna majengo ya kisasa ya parking
ambazo zinakua zimebanana na hivyo kuwapa uoga baadhi ya madereva kupaki gari
katikati ya magari mengine kwa kuhofia kugonga. Hili nalo tunashauliwa tuweke uoga
pembeni tujiamini na kufanya mazoezi taratibu na kwa tahadhari mpaka tutazoea.
Haipendezi unaingia kupaki unaomba msaada kwa mtu mwingine akuingizie gari hiyo
kwenye parking husika. - Kuegesha gari katikati ya gari zinafuatana. Hili ni tatizo kubwa kwa madereva wengi
kwa kua kukadiria kwetu ni tatizo na hali ya kutojiamini. Njia nzuri ya kupaki gari katikati
ya gari zilizofuatana ni kuingia kwa rivasi. Ikiingia kwa rivasi uwezekano wa kupaki gari
ikiwa imenyooka ni mkubwa kuliko kuingia kwa mbele inaweza kusababisha sehem ya
nyuma ibaki upande wa barabarani. - Uvumilivu. Tunatakiwa kua wavumilivu kwenye uzurmbe unaofanywa na madereva
wengine kwa kua ukiruhusu hasira ikutawale unaweza kujikuta unafanya mambo ya
ajabu na ukapata matatizo hapo barabarani. Mfano umekwazuraza na gari ya pembeni
yako inatakiwa uelewe kwamba ajali zipo kwa mtu yoyote anayetumia barabara hivyo
iwapo mtu kakugusa bahati mbaya lazima utumie busara kuzungumza naye na
kuyamalizq badala ya kutumia nguvu na matusi. Hii piq kwa wale ambao kukiwa na
foleni kidogo wanapiga honi akiona haitoshi anamfaya mwenzie kumtukana, hili pia si
jema na unaweza kupata matatizo ambayo hukuyategemea iwapo utakutana na mtu
mkorofi zaidi yako