Man City yafuzu robo fainali UEFA.

In Kimataifa, Michezo

Klabu ya Manchester City Jana usiku imekubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Fc Basel kwenye mchezo wa Marudiano wa klabu bingwa barani Ulaya.

Magoli ya FC Basel yamefungwa na  Elyounoussi na Lang huku goli la Man City likitupiwa na Gabriel Jesus.

Licha ya kupoteza mchezo huo Man City imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa tofauti ya goli 5-2.

Mchezo mwingine uliochezwa Jana ni kati ya Tottenham Hotspurs na wakongwe Juventus ambapo Spurs wamekubali kipigo cha goli 2-1 nyumbani na kutupwa nje ya michuano.

Spurs walikuwa wa kwanza kuona lango la Juventus kupitia kwa Son na baadae goli hilo kusawazishwa na Higuain kabla ya kinda wa Argentina Dybala kupigilia msumari wa ushindi.

Spurs imekuwa timu ya nne kuaga michuano hiyo yenye msisimko zaidi duniani baada ya FC Porto, PSG na Basel.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Jaji Mutungi avitahadharisha vyama vya siasa.

Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kutekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa kufuata na kuzingatia sheria na kanuni za vyama

Read More...

Bangi sasa ruksa Canada.

Canada imepitisha sheria rasmi kwa nchi nzima inayoruhusu matumizi ya bangi hadharani tofauti na hapo awali ambapo iliwabidi wananchi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu