MAOFISA AFYA WATAKIWA KUONGEZA UKAGUZI KWENYE MIPAKA

In Afya

Maofisa afya wanaofanya kazi kwenye mipaka nchini wametakiwa kuongeza umakini wa kufanya ukaguzi katika mipaka.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt. Zainab Chaula wakati alipotembelea mpaka wa Mutukula nchina Tanzania na Uganda ikiwa ni moja ya ziara yake ya kuangalia utayari wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko ambayo inafanywa na wizara ya afya kwa kushirikiana na TAMISEMI.

“Umakini mkubwa unatakiwa katika kufanya ukaguzi kwa wasafiri wanaopita kwenye.mpaka huu ingawa kuna mwiingiliano mkubwa baina ya nchi hizi mbili ili kuweza kuzuia magonjwa ya mlipuka kama Ebola usiingie nchini.

“Kujilinda ni jambo moja na kuzuia ni jambo lingine,nimetembelea mpaka huu, nimejionea na maofisa wetu wa Tanzania wa afya, forodha, uhamiaji wamenieleza changamoto iliyopo hapa ni mwingiliano mkubwa, watu wanatoka upande mmoja kwenda mwingine kwa wingi, wanashirikiana kwenye shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi,hivyo lazima muangalie tunatoka vipi kwenye hili.

Hata hivyo Dkt. Chaula aliwapongeza watumishi wote wa idara zote kwa ushirikiano na kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kudhibiti magonjwa ya milipuko hayajaingia nchini.

“Lakini pamoja na hayo, bado inahitajika muwe imara zaidi, ndiyo maana tumeleta vifaa tiba vya kisasa vya ukaguzi wa joto la afya ya mwili, nawasihi msimamie hili kwa umakini zaidi,” alisema.

Aidha, Dk. Chaula alisisitiza maofisa afya hao kuongeza elimu.ya afya kwa umma kwa wananchi wote wanaopita mpakani hapo ili kuwajengea uelewa jinsi ya kujikinga na dalili za magonjwa hayo

“Wataalamu wa afya wa Mkoa na viongozi wote pamoja hakikisheni elimu ya afya kwa umma inafika hadi kule vijijini, watu wetu waelewe jinsi ya kujikinga,” alisema Dk. Chaula.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tamisemi Yakanusha Taarifa Iliyotolewa Na Mgombea Urais Wa Chadema,tundu Lissu

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imekanusha madai yaliyotolewa na mgombea urais wa Tanzania

Read More...

Korea Kaskazini yaonya kuhusu shughuli za kijeshi la Korea Kusini kwenye eneo lake- KNCA

Korea Kaskazini imesema ilikuwa inautafuta mwili wa raia wa Korea Kusini aliyeuwawa na wanajeshi wake, lakini ikionya kwamba shughuli

Read More...

PICHA:Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bi. Ziada Sellah akizindua kitabu kinachoitwa “COVID-19 VITA VYA KARNE YA 19”

Wauguzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru-Arusha wakionesha vyeti vyao mara baada ya kutunukiwa vyeti

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu