Maonyesho ya Nane nane kuja kivingine.

In Kitaifa

Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kuitega amesema maonyesho ya wakulima, wavuvi, na wafugaji nane nane yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni yatakuwa ya tofauti na miaka mingine iliyopita kutokana na teknolojia za kisasa zilizopo.

Akizungumza na vyombo vya habari Mh.Kuitega amesema Mkoa wa Arusha umejipanga katika kuhakikisha maonyesho ya wakulima yanakuwa na wadau mbalimbali wakiwemo wa pembejeo, mifugo, kilimo, mbolea, taasisi za utafiti wa mazao ya kilimo na uvuvi

Amesema uwanja wa Themi wa nane nane uliandaliwa tokea miaka ya 93 ambapo kwa sasa viwanja hivyo vimetengwa kwa ajili ya sekta mbalimbali za mimea

Pia amesema mwaka huu ni maonyesho ya 25 ambapo ambapo ifikapo tar 22 wadau wataanza kuingiza bidhaa zao hadi ifikapo tar 29 mwezi huu ambapo yatafunguliwa tar 1 mwez wa 8 mwaka huu

Halikadhalika amewataka waalimu kuwaleta wanafunzi kwa wingi ili kuweza kujionea technolojia mpya na kufikia kauli mbiu ya Rais kuhusiana na Tanzania ya viwanda kwa lengo pia la kutimiza kwani uzalishaji katika mifugo na kilimo iongeze kasi viwandani

Waalimu wenye kuongoza makundi ya wanafunzi pia wafike kwa utaratibu maalumu ili kuweza kuepuka msongamano wa watu wengi kama miaka mingine iliyopita”Amesema Mh. Kuitega

Amesema piavwamejipanga hasa katika ulinzi na usalama ambapo wana mpango mzuri wa kusukuma maboresho ya kuonyesha bidhaa mbalimbali zinazoendana na mabadiliko ya teknologia na hatimaye kutoa fursa za ajira kulingana na technologia waliyoipata

Maonyesho hayo ni ya 25 ambapo yatafanyika katika viwanja wa Themi Njiro Mkoani Arusha ambapo mwaka huu yameambatana na kauli mbiu isemayo “WEKEZA KATIKA KILOMO UFUGAJI Na UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA”.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu