Maradona kuchunguzwa baada ya kumsifu Maduro.

In Kimataifa, Michezo

Shirikisho la soka la Mexico limeanzisha uchunguzi dhidi ya nguli wa zamani wa soka Diego Maradona kuhusu iwapo alikiuka kanuni za kimaadili baada ya kumsifu rais wa Venezuela Nicolas Maduro baada ya mechi iliyochezwa hivi karibuni. Maradona ambaye ni kocha wa timu ya daraja la pili ya Dorados ameibua sintofahamu kufuatia matamshi yake kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya Tampico Madero. Alisema anataka kuitoa mechi hiyo kwa ajili ya rais wa Venezuela Nicolas Maduro na raia wa Venezuela wanaoteseka kufuatia mzozo wa kimamlaka nchini humo. Taarifa ya shirikisho hilo, imesema kamati yake ya nidhamu imeanzisha uchunguzi dhidi ya matamshi hayo kwa madai kuwa yamekiuka vifungu vya 6,7,9,10 na 11 vya kanuni za maadili za shirikisho hilo. Maradona ni mshirika wa karibu wa Maduro na viongozi wengine wa siasa za mrengo wa kushoto wa Amerika Kusini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu