Marekani yaineemesha Tanzania.

In Uncategorized

SERIKALI za Tanzania na Marekani zimefanya mazungumzo kuhusu kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Mazungumzo hayo yamewakutananisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Uwekezaji, Geoffrey Mwambe na Balozi wa Marekani hapa nchini, Donald Wright.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana mara baada ya mazungumzo hayo, Profesa Mkumbo alisema katika kujenga ushirikiano na kushirikishana fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini, mazungumzo yao yalilenga kukuza biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Marekani.

“Leo (jana) tumekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini, Donald Wright kuona namna ya kukuza ushirikiano wetu wa nchi hizi mbili, tuna fursa nyingi na kubwa kwa wafanyabiashara wetu kunufaika fursa hizo,” alisema. Dk Mkumbo alisema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuweka jitihada za kuhakikisha nchi hizo mbili zinazidi kushirikiana katika nyanja za uwekezaji na kuleta manufaa na kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara na kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja.

Alisema pia wamezungumzia kuhusu mazao ya kimkakati hasa katika kuyachakata hapa nchini, kuuza bidhaa badala ya kuuza malighafi hasa matunda ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini. Kwa upande wake, Mwambe alisema pia wamezungumza kuhusu uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwamo ya afya hapa nchini.

“Wenzetu wanaonekana kuridhishwa na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika ya sekta ya uwekezaji na wawekezaji kutoka Marekani wameonesha wapo tayari kuja kuwekeza hapa nchini,” alisema.

Alisema tayari kuna kampuni imeonesha nia ya kuja kuwekeza katika sekta ya mawasiliano na kampuni ya utalii kutoka Arusha iliyoonesha nia ya kutaka kuongeza uwekezaji wake.

“Pia tumeongelea uchakataji wa mazao na ukiangalia Marekani inanunua korosho katika nchi nyingine na sisi tunauza korosho ghafi na hizo nchi zinachakata na kuuza Marekani, hivyo na sisi tunaweza kuzichakata hapa nchini na kuuza Marekani,” alisema.

Mwambe alisema pia yapo mazao mengine ya kimkakati kama kahawa na pamba ambayo yatachakatwa nchini na kuuzwa nje ya nchi na nchi kupata mapato kupitia kodi na kukuza ajira kwa wananchi katika viwanda vitakavyoanzishwa.

Naye, Balozi wa Marekani nchini, Wright alisema nchi hiyo itashirikiana kwa dhati na kwa karibu na serikali kuhakikisha wawekezaji kutoka Marekani wanawekeza Tanzania kutokana na kuwapo fursa nyingi za uwekezaji pamoja na hali nzuri ya ulinzi na usalama.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu