Marekani yakiwekea vikwazo kikundi kimoja cha jeshi la Iran.

In Kimataifa

Wizara ya fedha ya Marekani imekiwekea vikwazo kikundi kimoja cha jeshi la Iran pamoja na mtandao wa biashara unaokifadhili kikundi hicho.

Hii ni sehemu ya kampeni ya Marekani ya kuiwekea Iran shinikizo kubwa la kiuchumi.

Wakati wa kutangaza vikwazo hivyo wizara hiyo ya fedha imekituhumu kikundi hicho kwa kuwapeleka watoto wanajeshi nchini Syria kama uungaji mkono wa serikali ya rais Bashar al-Assad.

Kulingana na wizara hiyo ya Marekani, kikundi hicho kwa jina Basij kilichoundwa muda mfupi baada ya yale mageuzi ya mwaka 1979, ni mojawapo ya vikundi vinavyotumiwa na serikali ya Iran kuweka usalama wa ndani ya nchi na kina matawi katika kila mkoa na mji wa nchi hiyo.

Marekani inasema mbali na raia wa nchi hiyo Iran iliwasajili wahamiaji kutoka Afghanistan na Pakistan katika kikundi hicho kwa lazima jambo lililowafanya baadhi kutorokea Ulaya.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu