Marekani yamuonya Odinga dhidi ya kujiapisha Kenya.

In Kimataifa

Marekani imemtaka kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kuacha mpango wake wa kuapishwa kama rais wa nchi hiyo wiki ijayo.

Odinga aliwasilisha kesi juu ya mapungufu katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti katika Mahakama ya Juu nchini humo ambayo ilibatilisha uchaguzi huo na kuagiza uchaguzi wa marudio ufanyike.

Bw Odinga na muungano wake wa National Super Alliance hata hivyo walisusia uchaguzi huo wa 26 Oktoba ambapo Bw Kenyatta alitangazwa mshindi na mwishowe kuapishwa kwa muhula wa pili.

Waziri msaidizi wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika, Donald Yamamoto ambaye alikuwa amezuru Kenya alimtahadharisha Bw Odinga na pia akahimiza kuwepo mashauriano kati yake na serikali iliyopo madarakani.

Aidha alitahadharisha dhidi ya matendo ambayo yako nje ya katiba nchini humo.

Baadhi ya viongozi wa serikali wameonya kuwa tukio hilo la kuapishwa linaweza kuhusishwa na uhaini.

Mshauri wa Bw Odinga Salim Lone alipuuzilia mbali onyo hilo la Marekani na kusema Bw Odinga ataapishwa kama ilivyopangwa Jumanne wiki ijayo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu