Matokeo ya Uchaguzi: Dkt. Mollel Aibuka Kidedea Ubunge Siha.

In Kitaifa, Siasa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro baada ya Tume ya Uchaguzi (Nec), kumtangaza Dk Godwin Mollel kuwa mshindi wa kiti hicho.
Nec imemtangaza rasmi Dk Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi huo baada ya kupata kura 25,611 huku akiwaacha mbali wapinzani wake,  Elvis Mosi wa Chadema, Elvis Mosi aliyepata    kura 5,905 na mgombea wa CUF, Tumsifueli Mwanri aliyepata kura 274 huku Mdoe Azaria wa Sau akiambulia kura 170.
Kwa upande wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, hadi saa saba usiku shughuli ya majumuisho ya kura ilikuwa inaendelea lakini matokeo ya awali yaliyobandikwa na wasimamizi wasaidizi katika vituo mbalimbali vya kupigia kura, yanaonyesha kuwa mgombea wa CCM, Maulid Mtulia anaendelea kuongoza.
Mtulia anafuatiwa na mgombea wa Chadema, Salum Mwalimu pamoja na mgombea wa Cuf, Rajab Juma akifuatia kwa tofauti ya kura nyingi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu