Mauaji ya Kashoggi yalipangwa.

In Kimataifa

Mwendesha mashitaka mkuu wa Saudi Arabia Saud al-Mojeb amesema mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi yalipangwa. Taarifa hii inakinzana na iliyotolewa awali kwamba Khashoggi aliuawa kwa bahati mbaya akiwa kwenye ubalozi mdogo wa Saudia Arabia, nchini Uturuki. Maafisa wa Saudi Arabia awali walidai kwamba Khashoggi aliondoka ubalozini hapo. Kulingana na mwendesha mashitaka huyo taarifa hiyo iliyotolewa na Uturuki, inaashiria kwamba watuhumiwa wa mauaji ya Khashoggi walifanya kitendo hicho kwa kudhamiria. Msemaji wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema kwamba, kansela amezungumza na mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohammed Salman na kulaani mauaji hayo. Aidha ametaka kufanyika uchunguzi wa haraka, wa wazi na wenye kuaminika na wahusika kufikishwa mbele ya sheria.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu