May aairisha kura kuhusu Brexit.

In Kimataifa

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameahirisha kura iliyokuwa ifanyike leo bungeni kuhusu makubaliano ambayo serikali yake na Umoja wa Ulaya yalifikia kuhusu mchakato rasmi wa Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya ujulikanao Brexit. May ameahirisha kura hiyo kwa kuhofia kushindwa vibaya bungeni na kusema anaelekea Brussels, yaliko makao makuu ya Umoja wa Ulaya kufanya mazungumzo zaidi na viongozi wa umoja huo. Hata hivyo Umoja wa Ulaya umeonya kuwa hautaanzisha tena mazungumzo ya kufikiwa makubaliano mapya. May amekiri kuwa rasimu ya makubaliano aliyoyafikia na Umoja wa Ulaya mwezi uliopita ingepingwa na idadi kubwa ya wabunge iwapo ingewasilishwa bungeni leo Jumanne, lakini amesisitiza makubaliano hayo ndiyo bora zaidi ila atatafuta hakikisho zaidi hasa kuhusiana na suala tete la Ireland Kaskazini. Leo waziri huyo mkuu wa Uingereza atafanya mazungumzo na mwenzake wa Uholanzi Mark Rutte mjini The Hague kisha atafanya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin. Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk ambaye ameitisha mkutano maalum wa kilele wa viongozi wa nchi 27 wanachama wa umoja huo siku ya Alhamisi ameonya kuwa hawatajadili tena makubaliano yaliyofikiwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Majeshi ya Marekani yauwa raia Somalia

Majeshi ya Marekani yanayoendesha mashambulizi ya angani nchini Somalia dhidi ya ngome za wapiganaji wa Al Shabab nchini humo

Read More...

Idai yapoteza makazi ya watu 400,000.

Shirika la Msalaba Mwekundu linakadiria kuwa watu 400,000 wamepoteza makaazi yao nchini Msumbiji kutokana na Kimbunga Idai kilichoipiga nchi

Read More...

Baa la njaa kuikumba Kenya.

Zaidi ya watu milioni 1.5 nchini Kenya wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa kufuatia kutokuwepo kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu