May aunda mabaraza ya kibiashara kumshauri kuelekea Brexit

In Kitaifa

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameunda mabaraza matano mapya ya kibiashara kushauri kuhusu masuala yanayozikabili sekta muhimu za kiuchumi wakati ambapo nchi hiyo inajiandaa kujiondoa uanachama wa Umoja wa Ulaya, mchakato unaojulikana kama Brexit.Huku ikiwa imesalia chini ya miezi mitano kabla ya Uingereza kujiondoa rasmi kutoka umoja huo na mpaka sasa kukiwa hakujafikiwa makubaliano madhubuti kuhusu Brexit, viongozi wa kibiashara wa nchi hiyo wamekuwa wakitaka hakikisho kuhusu mustakabali wa kibiashara baada ya Brexit.May leo atakutana na mabaraza hayo mapya kujadili majukumu yao na masuala mengine ya kiuchumi kama uzalishaji, uwekezaji wa kimataifa na kumshauri kuhusu fursa na changamoto za kibiashara zitakazoikabili Uingereza katika siku za usoni.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Suzan Kiwanga afukuzwa Bungeni.

Spika wa Bunge, Job Ndugai jana alimtoa nje ya bunge, Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema) na kumtaka kutohudhuria

Read More...

Mtolea ajivua Uanachama wa CUF Akiwa Ndani ya Bunge Leo.

Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, kwa tiketi ya CUF ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu