Mbinu mpya TCRA kupambana na wezi wa mtandaoni.

In Kitaifa

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kulaba amezungumza na vyombo vya habari na kutoa mbinu mbadala kwa wananchi dhidi ya matapeli wanaotuma ujumbe wa simu wakiomba kutumiwa fedha katika namba fulani.

Amezungumza hayo pindi alipotembelewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa na kuwataka wateja wa mitandao ya mawasiliano kupuuza jumbe hizo huku mamlaka ya TCRA  ikiendelea kufanya uchunguzi wa kina kuwabaini wahalifu hao.

Kulaba amewataka wananchi kujielimisha wenyewe na kuwa waangalifu pindi wapokeapo ujumbe unaomtaka kutuma fedha.

Ametaja juhudi zilizofanyika na mamlaka ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na kutoa kitabu ambacho kimeeleza kinagaubaga matumizi ya simu na huduma zinginezo za mawasiliano zinavyopaswa kuwa.

”Ukipokea meseji ile na kwasababu zimezoeleka zipuuzeni, lakini sisi hatuishii kwenye kuzipuuza sisi tunafuatilia na hakuna atakayetuponyoka sasa tutakapo kamilisha mpango wetu tutawatangaza wahusika wote, tutawaweka kwenye vyombo vyenu muwafahamu, muwaseme wenyewe” Amesema Mbarawa.

Amesisitiza juu ya sheria kuendelea kuchukua mkondo wake dhidi ya wahalifu.

Aidha Mbarawa amesema TCRA iendelee kutoa taaluma kwa wananchi katika sekta hiyo na kuwasihi wateja endapo mtu atapokea ujumbe wa namna hiyo hatua ya kwanza ni kuripoti Polisi ili kuhakikisha wanasimamia vyema sekta hiyo ya mawasiliano.

Hayo yameelezwa kufuatia tabia iliyozuka hivi karibuni ya matapeli wachache wanaotumia mtandao vibaya kufanya utapeli wakiwemo waganga wa kienyeji.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mwanamfalme Saudia Kuchunguzwa kifo cha Khashoggi.

Kuna ushahidi kamili kwamba mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman na maafisa wengine wa ngazi za juu wanahusika kibinafsi

Read More...

Hafla ya kutambulisha tuzo ya serengeti yafanyika.

Waziri wa maliasilai na utalii Mh Hamis Kigwangala leo ameshiriki katika zoezi la utambulishwaji wa Tuzo ya Mbuga ya

Read More...

Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni 6.

Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza kupitia Jeshi hilo limeiomba Serikali kuwalipa deni la shilingi Bilioni 6.45 fedha zilizotumika

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu