Mbowe na Viongozi 8 wa CHADEMA wamkataa Hakimu.

In Siasa
Vigogo tisa wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wamewasilisha ombi la kutaka Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri kujitoa kusikiliza shauri lao.
Kufuatia ombi hilo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Julai 5, 2018 kutoa uamuzi katika kesi inayowakabili viongozi hao.
Uamuzi huo wa mahakama umetolewa jana Jumatatu Julai 2, 2018 na Mashauri baada ya  washtakiwa hao  kueleza sababu ya kutokuwa na imani nae.
“Baada ya kusikiliza sababu za washtakiwa walizotoa hapa mahakamani za kumtaka hakimu anayeendesha shauri hili kujitoa, Julai 5 mahakama hii itatoa uamuzi kama hakimu huyo ajiondoe kuendesha shauri hilo au asijiondoe” alisema hakimu Mashauri.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alisema wateja wake wamemueleza kuwa hawana imani na hakimu Mashauri anayeendesha kesi hiyo na wanaomba ujitoe kusikiliza shauri hilo, hivyo wanaomba nafasi ili waweze kueleza sababu za kutokuwa na imani nae.
Aliyeanza kueleza sababu za kutokuwa na imani na hakimu huyo ni Mbowe ambaye alidai kuwa ana sababu kumi.
Baada ya kupitia hoja za pande zote ambazo pia zilitolewa na washtakiwa wengine, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 5, 2018  atakapotoa uamuzi.
Washtakiwa katika Kesi hiyo  ni Mbowe, naibu makatibu wakuu, Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara); mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.
Wengine ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vicent Mashinji;  mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Washtakiwa kwa pamoja  wanakabiiwa na mashtaka 13.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Baraka da Prince sasa kufunga ndoa na Naj

Msanii wa Bongo fleva Baraka de Prince amebainsha wazi kufunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake Naj. Minong’ono ilikua

Read More...

Ajibuawataka Simba watulize boli, msimu ni wao

Nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu. Ajibu

Read More...

Waziri Mkuu kuzindua Daftari la kudumu la kupiga kura.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Dkt Athumani Kihamia, amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la Kupiga

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu