Mbowe: Tutakata Rufaa hata kama Sugu ameachiwa Huru.

In Siasa
Kufuatia  kuachiwa huru kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga kutoka Gereza la Ruanda, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, amesema bado hawajafahamu ni taratibu gani zimetumika kuwaachia huru wakati  kifungo chao kilikuwa bado.
“Katika mazingira ya kawaida, siku yao ya kifungo walichokuwa wamepewa kilikuwa kinaishia Juni 5, mwaka huu, lakini ghafla wakapewa taarifa kwamba wataachiwa leo. Hatuna hakika sana ni taratibu gani zimetumika kufupisha kifungo chao kwa sababu jambo hilo halijawekwa wazi.
“Tangu wamewekwa gerezani ni takribani miezi mitatu, mawakili wetu walifanya jitihada za kuhakikisha rufaa yao katika mazingira ya dharura inasikilizwa, lakini haikuwahi kupata jaji wala kusikilizwa kwa sababu kila jaji aliyepangiwa kesi hiyo alionekana ana udhuru,”alisema Mbowe.
Aidha, amesema wao wanaamini kesi hiyo haikuwa ya haki kwa sababu watuhumiwa walinyimwa dhamana mwanzoni, na kutokana na mazingira ya kesi yenyewe hawakutakiwa kupewa kifungo.
Pia amedai kwamba wataendelea na rufaa yao ili kuweka rekodi sawa na kudhihirisha kwamba Sugu na Masonga hawakuwa na makosa.
Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu