Mbunge wa Ukerewe, Joseph Michael Mkundi ajiuzulu Ubunge CHADEMA.

In Kitaifa
Mbunge wa Ukerewe, Joseph Michael Mkundi ametangaza kujiuzulu uanachama na nyadhifa zake zote ndani ya CHADEMA, na kuomba kujiunga CCM.

Miongoni mwa sababu alizotoa, ni kutopata ushirikiano kutoka kwa viongozi wenzake (CHADEMA) wakati wa ajali ya MV Nyerere.
“Chama cha Siasa kama Taasisi ya Umma na inayotoa maelekezo Kwetu wawakilishi wa Wananchi, yenyewe inapokuwa msingi wa Kujenga Chuki, uhasama, ubaguzi na Ukinzani na serikali. Taasisi hii inapoteza Uhalali wa Kiuongozi (leadership Legitimacy).
“Kwa Msingi Huo Leo Siku ya Jumatano tarehe 10 Oktoba 2018 natangaza kujivua uanachama wa Chadema na hii ikiwa kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema ibara ya 5.4.1,chama ambacho kwa Tiketi yake nilikuwa Diwani wa Kata ya Bukiko na Mbunge wa Jimbo la Ukerewe
“Natangaza kuomba Kujiunga na CCM, Chama ambacho kwa hakika nimeona wakidhihirisha kwa Vitendo Itikadi yao ambayo imejengwa katika misingi ya Utu, Undugu, Mshikamano, Haki na Umoja wa watu wa Tanzania” –Joseph Michael Mkundi 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Kitambulisho cha Vladimir Putin cha ujasusi chapatikana Ujerumani.

Kitambulisho cha Vladimir Putin alichopewa kama jasusi Ujerumani alipokuwa anafanya kazi kama jasusi wa Urusi kimepatikana katika makavazi mjini

Read More...

May aairisha kura kuhusu Brexit.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameahirisha kura iliyokuwa ifanyike leo bungeni kuhusu makubaliano ambayo serikali yake na Umoja

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu