Messi aifikisha Barcelona kwenye rekodi iliyodumu miaka 38 La Liga

In Kimataifa, Michezo

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi jana usiku amefanikiwa kuifikisha klabu yake kwenye rekodi iliyokuwa inashikiliwa na klabu ya Real Sociedad ya kucheza mechi 38 kwa msimu mmoja bila kupoteza.

Magoli matatu pekee (Hat-Trick) kutoka kwa Messi dhidi ya Legannes (3-1) ndiyo yameifanya Barcelona kufikia rekodi hiyo ambapo hakuna klabu nyingine iliyowahi kufanya hivyo zaidi ya timu hizo mbili.

Klabu ya Sociedad iliweka rekodi hiyo miaka 38 iliyopita kwenye msimu wa mwaka 1979/80 ambapo toka wakati huo klabu iliyofuata kucheza mechi nyingi bila kufungwa ni Real Madrid na Barcelona zote zilifikisha mechi 31 kwenye msimu wa 1988/89 na 2010/11 .

Mchezo unaokuja Barcelona watachuana na klabu ya Valencia, mchezo ambao utaamua kama rekodi hiyo itavunjwa na Barcelona au itasalia kama ilivyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Bunge lawataka Heche na Zitto Kuripoti Polisi.

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amemtaka Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) na Mbunge wa Kigoma

Read More...

Kiongozi wa Kiroho matatani kwa ubakaji.

Kiongozi wa Kiroho wa India maarufu kama Guru anayedaiwa kuwa na mamilioni ya wafuasi duniani amekutwa na hatia ya

Read More...

UEFA: Mo Salah, Mane na Firmino wasababisha vilio Italia.

Klabu ya soka ya Liverpool usiku wa jana imefanikiwa kuingiz mguu mmoja katika hatua ya fainali ya klabu bingwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu