Messi aiokoa Barcelona Uingereza, Avunja rekodi yake mbovu dhidi ya Chelsea.

In Kimataifa, Michezo

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi jana usiku amefanikiwa kuiokoa klabu yake kutoka kwenye kipigo kwa kuisawazishia goli 1-1 dhidi ya mabingwa wa Uingereza Chelsea kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya.

Lionel Messi na Andres Iniesta

Goli hilo la kusawazisha la Messi limevunja rekodi mbovu ya mchezaji huyo ya kutofunga goli lolote dhidi ya Chelsea pindi timu hizo zinapokutana akiwa na timu yake kwa zaidi ya miaka 7.

Imemchukua mchezaji  huyo dakika 730 na mechi 9 kufunga bao lake la kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya (UEFA).

Messi ambaye amekuwa yuko katika kikosi kimoja na Andres Iniesta tangu aanze kuichezea Barcelona mpaka sasa, alikuwa hajawahi kuzigusa nyavu za Chelsea, hadi Jana usiku ilipomlazimu kutumia dakika 75 uwanjani kupata goli hilo.

Iniesta ndiye aliyemsaidia Messi kufunga bao hilo kwa pasi safi ya mwisho kunako dimba la Stamford Bridge.

Goli la Chelsea lilifungwa na Willian kunako dakika ya 62 kwa shuti zuri lililopita miguuni mwa mabeki wa Barcelona.

Kwa sare hiyo Barcelona imekuwa na faida ya goli moja la ugenini, kabla timu hizo hazijakutana tena katika mchezo wa marudiano utakaochezwa kwenye Uwanja wa Camp Nou, Jumatano ya March 14 2018.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu