Meya Aagiza Halmashauri Ziajiri Watu wa Kuzika Wafu Waliokosa Ndugu Dar.

In Kitaifa
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezitaka halmashauri zote jijini hapa kuajiri watumishi ambao watakuwa wanafanya kazi ya kuzika miili ya watu ambao watabainika kuwa hawana ndugu.

 

Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa, Machi 21, 2018 kwenye kikao cha robo ya pili ya Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam ,ambapo amewaeleza madiwani hao kuwa jukumu la kuzika marehemu wasiokuwa ndugu ni la jiji, kwakushirikiana na halmashauri hivyo wanapaswa kuwajibika katika hilo.
Amefafanua kuwa hadi sasa jiji limeshanunua gari pamoja na mahitaji mengine ya kuhifadhia miili hiyo pindi inatokea na kwamba changamoto iliyopo ni watu ambao watashirikiana kutekeleza jukumu hilo.
“ Mtakuabliana na mimi kwamba tulishakubaliana kwamba jambo hili lifanyike kwenye halmashauri zetu, lakini hadi sasa Kinondoni pekee ndio wametimiza agizo hili, sasa ninaagiza tena halmashauri nyingine za jiji hili kuajiri watu hao” amesema Meya Mwita.
Mwita amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na halmashauri nyingine zilizopo jijini hapo walikubaliana kuzika watu wasiokuwa na ndugu hivyo kila mmoja anapaswa kutekeleza makubaliano hayo.
“Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzikwa na jiji, natulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda,” amesema.
Amefafanua kuwa watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa, wanapokaa hospitalini zaidi ya siku 20,jiji linalazimika kuwazika hivyo wapo ambao wanazikwa kwenye halmashauri mbalimbali.
Hivyo wakati Jiji la Dar es Salaam likitimiza wajibu wake katika kuzika marehu hao kila halmashauri linajukumu la kutoa watumishi kwa ajili ya kuzika.
Amefafanua taarifa alizonazo ni Halmashauri ya Kinondoni pekee ndio ambayo imeajiri watumishi kwa ajili ya kuzika miili ya watu ambao wamefariki na hawana ndugu.
“Ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha wanafanikisha kupatikana kwa watumishi hao haraka,” amesema Meya Mwita.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu