MFUKO WA TAIFA WA BIMA WA AFYA NHIF WAZINDUA VIFURUSHI VITATU VYA AFYA AMBAVYO NI NAJALI AFYA, WEKEZA AFYA, NA TIMIZA AFYA

In Afya

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho gambo leo amezindua vifurishi vitatu vya mfuko wa taifa ya afya wa NHIF katika viwanja vya mbauda kata ya Sombetini jijini Arusha

Akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi huo mkuu wa mkoa amesema kuwa, mkoa wa arusha umejipanga kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya ili kuwasaidia katika upatikanaji wa matibabu kiurahisi.

Aidha amewataka amesema serikali ina mkakati wa kuboresha huduma za afya kwa kujenga vituo vya afya kila mkoa ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo ambapo mfuko wa afya ni njia mojawapo ya kurahisisha huduma hizo kwa wananchi kwa kuepuka gharama za matibabu

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya bima ya afya Tanzania Mh. Anna Makinda amesema kuwa, huduma hiyo ilianzwa mwaka 2011 lengo likiwa ni kurahisisha huduma za matibabu na wananchi wa hali ya chini kunufaika na huduma hizo,

Amesema kuwa mfuko huo utamlenga kila mtu wakiwemo, watoto, wazee, wajasiriamali, na familia kwa ujumla

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa taifa wa afya NHIF Bernard Konga amesema kuwa, vifurushi hivyo vinegawanyika mara tatu ambavyo ni jali afya, wekeza afya, na timiza afya,

Nao baadhi ya wananchi waliyohudhuria kwenye uzinduzi huo wameishukuru serikali kwa kuanzisha mfuko huo kwani vitasaidia kurahisisha huduma za matibabu

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu