Mfumuko wa bei Mwezi Uliyoisha wabaki asilimia 3.8

In Kitaifa

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwezi Uliyoishia Desemba 2019 umesalia kuwa asilimia 3.8,kama ilivyokuwa mwezi wa Novemba mwaka 2019
Hiali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidjhaa na huduma kwa mwaka uliyoishia Mwezi desemba 2019 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka uliyoishia Novemba 2019

Akizungumza na Vyombo vya habari Katika ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoani Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu kwa Jamii ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) bi,Ruth Davison Mfumuko huo kusalia hivyo ,kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula na bidhaaa zisizokuwa za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi desemba mwaka 2019, zikilinganishwa na mwezi kama huo mwaka 2018.

Miongoni mwa bidhaa za vyakula zilizoongezeka mwezi desemba mwaka 2019 zikilinganishwa na mwezi kama huo mwaka 2019,ni Mchele kwa asilimia 7.0,Mtama kwa asilimia 3.3, nyama kwa asilimia 2.3, Maharagwe kwaa asilimia 7.7 na Viazi Mviringo kwa asilimia 2.1,Mafuta ya taa kwa asilimia 7.1,jiko la kupikia la gesi kwa asilimia 1.6 Mafuta ya Petroli kwa asilimia 8.7 na disdeli kwa asilimia 8.7.

Aidha,kwa upande wa bidhaa zaa vinywaji baridi amesema kuwa kwa mwezi uliyoishia desemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1

Ruth amefafanua kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kutoka mwezi January hadi desemba 2019 ,umepungua hadi asilimia 3.4 mwaka uliyoishia 2019,kutoka asilimia 3.5 mweze wa desemba 2018.

Hata hivyo wastani wa stani wa bidhaa za vyakula umeongezeka hadi asilimia 4.3 mwaka 2019 kutoka asilimia 3.7 mwaka 2018.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za soka Ulaya.

Inter Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa N'Golo Kante huku Blues wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili

Read More...

Manchester City kushiriki kombe la Ulaya.

Klabu ya Manchester imefanikiwa kubadili marufuku ya miaka miwili kushiriki katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya kuanzia msimu

Read More...

Mama akiri kuua Watoto wake wanne.

Mwanamke mmoja nchini Kenya Betrice Mwende, anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne, amekiri Mahakamani kuwa ni

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu