Mgogoro Sudan wazuka upya baada ya wanajeshi kuwashambulia waandamanaji.

In Kimataifa

Vikosi vya ulinzi nchini Sudan vimetumia nguvu kujaribu kuwatawanya waandamanaji waliokita kambi nje ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum.

Kwa mujibu wa waandamanaji hao, milio ya risasi imekuwa ikisikika na tayari watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa kwenye rabsha hizo.

Sudan imekuwa chini ya utawala wa Baraza la Kijeshi la Mpito toka Rais Omar al-Bashir alipinduliwa mwezi Aprili.

Waandamanaji wamekuwa wakilazimisha utawala urejeshwe mikononi mwa serikali ya kiraia.

“Kwa sasa kuna jaribio la kutawanya waandamanaji waliokita kambi,” imeeleza taarifa fupi kutoka kwa Jumuiya ya Wataalamu wa Sudani ambao ndio waratibu wa maandamano hayo ya kitaifa.

Mashuhuda wanasema kuwa kwa sasa waandamanaji wanachoma matairi na kuweka vizingiti ili kuwazuia maafisa usalama kuwafikia.

Inaripotiwa kuwa mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu