Mgombea urais wa chama tawala Burundi atangazwa mshindi kwa kupata asilimia 68.7

In Kimataifa

Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ametangazwa mshindi leo kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimedaiwa kukumbwa na visa vya udanganyifu. Ndayishimiye ametangazwa kushinda baada ya kupata asilimia 68.72 ya kura zilizopigwa. Tume ya uchaguzi nchini Burundi ambayo imetangaza matokeo hayo moja kwa moja kupitia vyombo vya habari nchini humo, imesema Agathon Rwasa wa chama cha National Freedom Council (CNL) ambaye ndiye mshindani mkuu wa Ndayishimiye amepata asilimia 24.19 ya kura. Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, asilimia 87.7 ya wapiga kura waliojiandikisha walishiriki uchaguzi huo. Hapo awali, msemaji wa Rwasa alisema kilichotokea kwenye uchaguzi huo ni mpango uliosukwa vyema na chama tawala wa kung’ang’ania madaraka.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Manchester City kushiriki kombe la Ulaya.

Klabu ya Manchester imefanikiwa kubadili marufuku ya miaka miwili kushiriki katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya kuanzia msimu

Read More...

Mama akiri kuua Watoto wake wanne.

Mwanamke mmoja nchini Kenya Betrice Mwende, anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne, amekiri Mahakamani kuwa ni

Read More...

Mtoto wa Nelson Mandela afariki dunia.

Zindzi Mandela, mtoto wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela na aliyekuwa balozi wa Afrika Kusini nchini

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu