Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Aula apewa milioni 100 na Rais Magufuli.

In Kitaifa
Mgunduzi wa madini ya Tanzanite, Jumanne Ngoma ametoa ya moyoni baada ya Rais John Magufuli kusema Serikali inautambua mchango wake na kumpa Sh 100 milioni.
Mtoto wa Jumanne Ngoma akizungumza baada yakupata nafasi.
Akizungumza leo Aprili 6, wakati wa uzinduzi wa ukuta kuzungumza mgodi wa Tanzanite, Magufuli amesema atampa barua Mzee Ngoma ya kutambua mchango wake katika ugunduzi wa madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee.
Mtoto anayetoka katika familia ya mzee ngoma akimshukuru Rais kwa kumkumbuka Mzee Ngoma.
Mzee Ngoma alimshukuru Rais Magufuli na kusema alibaini kuwa kiongozi huyo amechaguliwa na Mungu tangu wakati wa kampeni za urais mwaka 2015.
“Ninakushukuru sana Rais, kwa heshima hii na kunitambua mimi kama mgunduzi wa madini, ni heshima kubwa kwangu na niseme kuwa wewe umechaguliwa na Mungu,” amesema na kuongeza:
“Wananchi wa Mirerani huyu ni Rais wa wanyonge, mimi nisingejulikana leo hii, hii ni furaha kubwa.”
 Mtoto wa Mzee Ngoma, Asha Ngoma naye ametoa neno katika hafla hiyo na kumshukuru Rais kwa kuusoma na kuufanyia kazi ujumbe wake wa simu aliomtumia Rais leo asubuhi saa 12 kasoro.
“Nikushukuru sana kwa sababu sikutegemea kama utausoma na kuufanyia kazi ujumbe wangu wa simu niliokutumia leo asubuhi. Naomba uendelee kuuthamini mchango wa mzee Ngoma na kuhakikisha madini ya Tanzanite yanaendelea kuwa na thamani,” amesema.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu