Mikoa na Halmashauri Yaagizwa Kuzuia Matukio ya Moto Mashuleni

In Kitaifa

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya kuhakikisha matukio ya moto katika shule zenye mabweni yanazuiliwa ili kutoathiri taaluma.

Mhandisi Nyamhanga ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea shule ya sekondari Endasaki mchanganyiko na shule ya sekondari ya wasichana Nangwa zilizopo wilayani Hanang ambapo amesema matukio ya moto katika shule za sekondari nchini yanatokana na hujuma, hitilafu za umeme na matumizi mabaya ya vifaa vya umeme ambavyo vinaleta hitilafu katika mifumo ya umeme na kusababisha moto.

“kumekuwepo na matukio ya mabweni katika shule za sekondari kuchomwa moto, sisi kama Serikali hatupendi kuona matukio hayo, hivyo basi ulinzi uimarishwe hasa maeneo ya shule, ni lazima mabweni yafungwe wanafunzi wanapotoka, pia matumizi ya umeme kwa wanafunzi kwa vifaa kama pasi yadhibitiwe”

Nyamhanga pia ameutaka Uongozi wote wa Mkoa, Wilaya, Kata na shule kuchukulia suala la ulinzi mashuleni kwa ukaribu ili kuzuia uhalifu huo na kuondoa hofu na kutoathiri wanafunzi wanapokuwa masomoni.

Aidha, amepongeza kiwango cha ufaulu kwa shule ya sekondari ya wasichana Nangwa na sekondari ya Endasaki na kuwataka walimu na wanafunzi kuongeza bidii katika kufundisha na kusoma na kwamba Serikali itaendelea kutenga fedha kupitia programu zake na Wadau kama EP4R, EQUIP-T, Tusome pamoja na Mpango wake wa Elimu Bila Malipo ambapo kiasi cha fedha shilingi 28.5 Bilioni hupelekwa mashuleni moja kwa moja kila mwezi.

Nyamhanga pia ameagiza kukamilika kwa maboma ya shule za msingi na sekondari kabla ya tarehe 30 Juni, 2019 ili kuongeza idadi ya vyumba vya madarasa lakini pia kuhakikisha madawati yanawekwa katika kila chumba cha darasa kinachomalizika kujengwa.
Naye Mkuu wa shule Endasak Gisela Msofe amesema
wanaishukuru Serikali kwa kutoa fedha kiasi cha 24,500,000.65 kwa kujengea maboma ya vyumba viwili vya madara lakini pia shilingi 60,000,000.00 kutoka Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa matatu pamoja na viti na meza zake.

Mhandisi Nyamhanga amehitisha ziara yake wilayani Hanang kama ziara yake ya kawaida ya kikazi kujionea hali ya utoaji wa huduma kwa wananchi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Miss Tanzania Mikononi mwa Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka mshindi wa shindano la urembo Tanzania (Miss Tanzania) kwa mwaka 2019 Sylivia Bebwa, kuhakikisha

Read More...

Magufuli ampandisha cheo Brigedia Jenerali Charles Mbuge.

Rais Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT. Mbuge anachukua nafasi Meja Jenerali Martin Busungu ambaye

Read More...

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE.

Juventus imekataa kumuuza winga Douglas Costa 28 licha ya Man United kuwa na hamu ya kumsajili baada ya mkufunzi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu