Miss Tanzania Mikononi mwa Waziri Mkuu

In Kitaifa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka mshindi wa shindano la urembo Tanzania (Miss Tanzania) kwa mwaka 2019 Sylivia Bebwa, kuhakikisha anakuwa Balozi mzuri wa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali na aishi kwa kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana ofisini kwake jijini Dodoma, alipokutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, waandaaji wa shindano ya Miss Tanzania pamoja na mshindi wa Kwanza, wa pili na Watatu wa shindano hilo. “Miss Tanzania lazima awe mbunifu na uelewa mpana katika masuala mbalimbali zikiwemo jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya wananchi kama kuhamasisha elimu hususan kwa watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao”, amesema Waziri Mkuu.

Ameongeza kuwa, Miss Tanzania anatakiwa kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini, shughuli zinazofanywa na Serikali katika kukuza uchumi pamoja na kuhamasisha wananchi washiriki katika kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amempongeza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Mwakyembe kwa namna anavyoratibu shughuli mbalimbali katika wizara hiyo, kwa kuwa hata katika sekta ya michezo viwango vimeanza kuonekana.
Amesema Serikali inaunga mkono masuala ya michezo na inapenda kuona viwango vinapanda, hatua ambayo itawawezesha wahusika kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki.

Kwa upande wake, Waziri Mwakyembe amemshukuru Waziri Mkuu kwa kukubali kuonana na ujumbe huo hususani Miss Tanzania, ambaye anajiandaa kwenda kushiriki shindano la urembo la Dunia (Miss World) linalotarajiwa kufanyika London, Uingereza Disemba 14 mwaka huu.

Naye Miss Tanzania 2019, Sylivia ameishukuru Serikali kwa fursa aliyopewa ya kukutana na Waziri Mkuu na kuongeza kuwa atajitahidi kuhakikisha anatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwemo kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano hilo la Miss World na kwamba anakwenda kutumia lugha ya kiswahili.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

David Luiz kuitangaza Rwanda Kimataifa.

Mchezaji wa klabu ya Arsenal, David Luiz ameahidi kuitangaza Rwanda kimataifa kwenye sekta ya utalii kwa marafiki zake wanaoishi

Read More...

Rekodi yawekwa na Kipchoge kutoka Kenya

Eliud Kipchoge amekuwa Mwanariadha wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini

Read More...

Habinder Seth aandika barua kwa DPP kukiri makosa yake.

Habinder Seth, anayekabiliwa na makosa ya Uhujumu Uchumi amemuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kukiri makosa yake na

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu