Mjadala wa kanuni ya idadi ya wachezaji wa kigeni waleta mkanganyiko

In Michezo

Kocha mkuu wa kikosi cha Ihefu FC kinachoshiriki ligi daraja la
kwanza Maka Mwalwisi amesema mjadala wa kanuni ya idadi
ya wachezaji wa kigeni katika klabu za ligi kuu, umekuwa
kichocheo cha kuleta mkanganyiko kwa wadau wa soka nchini
ambao bado hajafahamu nini wanakihitaji.


Mwalwisi amesema miaka nenda rudi watanzanaia wamekua
wakishindwa kutabua nini wanachokihitaji katia mjadala huo
ambao umewahi kuibuliwa zaidi ya maramoja, kutokana na
baadhi yao kuwa pamoja kwa wakati fulani na wengine kupinga.
Amesema kiuhalisia soka la Tanzania linahitaji usaidizi mkubwa
katika mjadala huo na kila mmoja anpaswa kufikiria kwa kina,
na sio kujadili kwa kuangalia maslahi ya klabu ama timu
anayoishabikia.
1
Kocha huyo ambaye aliwahi kuwa msaidizi wa kocha Juma
Mwambusi wakati akiwa mkuu wa benchi la ufundi la Mbeya
City zaidi ya miaka mitatu iliyopita, amesema kiuhalisia mdajala
wa wachezaji wa kigeni una maslahi ya taifa kutokana na

kuzigusa klabu kubwa ambazo hutoa wachezaji wanaokwenda
kwenye kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars).
Amesema kwa upande wake anaamini hoja ya waziri mwenye
dhama Harrison Mwakyembe ambayo imezua mjadala, ina
mashiko na inapaswa kupewa nafasi ya kuangaliwa kwa kina
kwa maslahi ya Taifa Stars ya baadae.

Kocha Mwalwisi hakuishia hapo, pia akagusia upande wa
viongozi wa vilabu vya soka nchini kwa kusema wamekua
kichocheo kikubwa cha kuwadharau wachezaji wazawa, na
kuwatahamini wachezaji wa kigeni jambo ambalo linaendelea
kuwadidimiza watetezi wa Taifa Stars.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu