Mjasiriamali Mwanamke ampongeza Rais Magufuli

In Kitaifa

Mjasiriamali Mwanamke msomi jijini Arusha ambaye anamiliki kiwanda cha kutengeneza na kuzalisha vitafunwa kijulikanacho kama MATTO BEKARY kilichopo Njiro jijini Arusha amempongeza raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tazania Dr. Magufuli kwa kuhimiza Tanzania ya viwanda kwani imesaidia kuamsha wanawake na vijana kujitegemea

Mwanamke huyo ambaye ni Neema Matto amesema kuwa kiwanda hicho kina takribani miaka 3 ambapo kimekuwa kikizalisha Mikate, Maandazi, cake, na Cooks amesema kuwa ameweza kuthubutu kutumia fursa hiyo na kuona mafanikio mazuri sana

“Mikate yangu  ina ladha tofauti na mikate mingine na wateja wangu wamekuwa wakiidurahia sana na nimekuwa nikisambaza bidhaa hizo, madukani na super market sambamba na kuifikia jamii nyumva kwa nyumba kwa kuwa inakubalika na gari maalumu la kusambaza maeneo mbalimbali jijini Arusha na  ina virutubisho vyote vya mwili”Amesema mama Matto

Amesema kuwa nafasi ya mwanamke kwenye kiwanda chake anaweka kipao mbele kwa kuwa mwanamke ni jeshi kubwa lakini pia ameweza kuwaajiri zaidi ya vijana kumi 10 kiwandani hapo ambapo ni njia mojawapo ta kuondoa changamoto ta ajira kwa vijana na pia kuweza kushirikiana vizuri na familia yake kusomesha watoto na mambo mbalimbali ya maendeleo

Amesema kuwa changamoto anazokabiliana nazo ni pamoja na watanzania kutodhamini bidhaa za ndani na kuchukua za nje bila kujua vuna virutubisho vyote, na pia ni njia mojawapo ya kuwaunga mkono wajasiriamali wa ndani, na pia umeme kukatika ba kusabababisha unga kuharibika, na pia biashara kutokuwa nzuri kutokana na changamoto ya virusi vya coroño ambavyo vimesababisha biashara kuyumba lakini kuanzia mwezi wa 7 biashara itakuwa vizuri zaidi

Kijana Isaya Vunia ni kijana ambae amefanya kazi ya kuoka mkate kwa mda wa miaka 3 kwenye kampuni hiyo ambapo amesema kutokana na ajira hiyo ameweza kufanya mambo mbalimbali ta kimaendeleo kama kutunza familia yake na kuwasaidia watu wasiojiweza pia amemshukuru Neema kwa kumpa nafasi kwenye kiwanda hicho kwani atafikia malengo yake akitoka hapo

Amesema kazi yake kubwa ni kuhakikisha anatengeneza vitafunwa vilivyo bora na kuhakikisha swala la usafi kwenye kiwanda hicho linazidi kuboreshwa kwani wana mavazi maalumu ya kuvaa wakiwa ndani ya kiwanda hicho na mashine za kisasa ili kutoruhusu bakteria kuingia ndani ya kiwanda

Hata hivyo Neema amewataka watanzania kununua bidhaa hizo kwa kuwa zina ubora na zina faida mwilini ikiwa ni pamoja na kumuunga mkono ili aweze kuifikia jamii kwa kuweza kusambaza kwa urahisi

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu