Moto mkubwa waunguza msitu, watu 20 wafariki Ugiriki.

In Kimataifa

Moto mkubwa uliozuka na kuunguza msitu nchini Ugiriki umeua watu 20, huku mamlaka nchini humo zikisema kuwa zinahitaji msaada wa kimataifa ili kukabiliana na moto huo.

Mamia ya wafanyakazi wa vikosi vya zima moto,wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo,huku watu wakiwa wameyakimbia makazi yao katika maeneo ya karibu na mji mkuu wa taifa hilo Athens.

Watu 104 wamejeruhiwa kati yao 11 wakiwa katika hali mbaya, lakini watoto 16 nao wamejeruhiwa.

Waziri mkuu Tsipras amesema hali ya hatari imetangazwa katika Attica karibu na mji wa Athens.

Nchi za Italia, Ujerumani, Poland na Ufaransa wametuma misaada ya ndege, magari na watalaamu wazima moto.

Mati, Athens, Ugiriki, 23 Julai 2018
Wengi wa waliofariki walikuwa katika mji wa pwani wa kitalii wa Mati, kaskazini mashariki mwa Athens

Huu ndio moto mbaya zaidi wa nyikani kukumba Ugiriki tangu mwaka 2007 pale watu kadha walippouawa na moto rasi ya Peloponnese kusini mwa nchi hiyo.

Rafina, Athens, Julai 23, 2018.
Image captionWakazi wametakuwa kuhama nyumba zao
Neo Voutsa, kaskazini mashariki mwa Athens, Ugiriki, 23 Julai 2018.
Image captionWaziri Mkuu Alexis Tsipras amesema wazima moto wote wameitwa kukabiliana na moto huo
Moto Kineta, karibu na Athens, Julai 23, 2018
Image captionNyumba nyingi zimeharibiwa na moto huo

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Msako mkali dhidi ya makanisa ya kikristo umeanza China na kuzua taharuki

Hatua ya hivi karibuni ya msako mkali unaotekelezwa na polisi dhidi ya makanisa nchini China umesababisha taharuki kubwa kwamba

Read More...

Mshauri wa zamani wa usalama wa Trump kuhukumiwa.

Mshauri wa zamani wa usalama wa taifa nchini Marekani Michael Flynn anatarajiwa kuhukumiwa leo katika mahakama kuu mjini Washington

Read More...

Jose Mourinho atimuliwa Manchester United.

Jose Mourinho amefutwa kazi wadhifa wake kama meneja wa Manchester United. Klabu hiyo imetangaza kwamba ameondoka katika klabu hiyo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu