Mrembo aliyechora tatoo ya Gentriez afariki dunia akiwa India.

In Burudani

Msanii wa Bongo Fleva kutokea Arusha Gentriez Mwakitabu ameonyesha hisia kali kwa mwanamke anayefahamika kwa jina la Lisa almaarufu Gagalious gaga aliyechora tatoo ya picha yake kwenye mwili wake na sasa amefariki.

Akiongea na Funiko Base ya Radio 5 Gentriez amesema alifahamiana na msichana huyo mrembo miaka 6 iliyopita kupitia mtandao wa Fafebook, na mawasiliano yao ya mtandao yalikomaa na hatimae wakawa Wachumba kupitia mtandao kwa kipindi hicho na baadae msichana huyo alienda masomoni India.

” kutokana na long distance iliyokuwepo tukapotezeana yeye akamove on na Maisha yake na mimi nikaendelea na Maisha mengine pia, lakini alikua bado ana love na mimi alikua ananikubali sana sababu alikua anapenda kazi zangu lakini hatukuwahi kumeet hata siku moja”.Alisema Gentriez

“Tatoo yangu aliichora kama miaka 2 iliyopita lakini mimi tayari nilishamove on na Maisha yangu, lakini akasema hata kama umemove on mimi bado nakukubali”.Alisema Gentriez

Gentriez ameiambia Funiko Base mara ya mwisho kuwasiliana nae ni miezi 2 iliyopita na sasa hivi amefariki na chanzo cha kifo cha gagalicious alianza kuumwa muda mrefu sana akiwa India mapafu yake yalipata hitilafu alikua akitumia madawa ya kulevya pamoja na kutumia vilevi vikali.

Baada ya muda alipata nafuu na kurudishwa Nyumbani Arusha Mwezi wa tano na Umauti ndipo ulipomkuta na Msiba upo Kijenge Sterio.

Gentriez amendika kwenye page yake ya insta nakusema;πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

My condolence to your family & friends,upendo wako haukuwa wa kawaida hasa ukizingatia hatukuwahi hata kukutana but umekuwa na upendo kwangu mpaka kufikia hatua ya kuchora tattoo ya picha yangu kwenye mwili wako kitu ambacho sio kila mtu anaweza kufanya. Rest In Peace my dear friendπŸ™πŸΎ @gagalious_gaga

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mufti Mkuu wa Tanzania aomba kutokomea kwa Corona.

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Zubery Bin Ally amewaomba watanzania kuungana kwa pamoja kumuomba mwenyezi Mungu ili virusi vya

Read More...

Simba waendelea kula mifugo Mara.

Serikali Wilayani Serengeti Mkoani Mara imekiri kuwepo kwa kundi la Simba linaloendelea kula mifugo ya wananchi katika wilaya

Read More...

Amjeruhi mpenzi wake kwa risasi wakiwa hotelini…

Polisi mkoani Geita inamshikilia mfanyabiashara Bw.Salum Othman mkazi wa jijini Mwanza kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumpiga risasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu