Msanii wa Kenya, Jaguar akana shitaka la kuua vijana Wawili

In Burudani

Mwanamuziki Mashuhuri Nchini Kenya, Charles Njagua Kanyi anayejulikana Kisanii kwa jina la Jaguar amekana shitaka la kusababisha Vifo vya vijana wawili waendesha bodaboda kufuatia ajali iliyosababishwa na gari lake aina ya Range Rover Spot.

Katika ajali hiyo iliyotokea march 21 mwaka huu katika barabara ya sagana Makutano, ilisababisha Vifo vya watu wawili ambapo alikuwa mwendesha bodaboda na abiria wake.

Jaguar awachiliwa kwa dhamana ya shilingi 50,000 na mahakama ya Kirinyaga
Gari la Jaguar likiwa katika eneo la ajali hiyo

Akijibu Shtaka hilo jana Jumanne ya tarehe 11 katika mahakama ya Baricho iliyopo eneo la Kirinyaga, Pamoja na uchunguzi kuendelea kufanyika Jaguar alikana shtaka hilo akiwa na ujasiri wa kutosha tofauti na wiki tatu zilizopita ambapo pia alisomewa shitaka hilo na kuonekana kama mtu mwenye wasiwasi na mawazo muda wote akiwa mahakamani.

Jaguar ambaye anagombea Ubunge katika eneo bunge la Starehe ameonekana kupata upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wakisema kwamba amejiharibia kwa tukio hilo japokuwa yeye bado anaamini kwamba katika uchaguzi huo wa mwaka huu ataibuka Kidedea na kuingia Bungeni.

Kwa upande wa familia za waliopoteza maisha zinataka haki itendeke kwa usawa bila kuangalia jina la Jaguar na heshima aliyonayo katika Nchi ya Kenya.

Hata hivyo Jaguar aliachiwa kwa dhamana ya sh. 50,000 za kenya sawa na  shilingi 120,000 ya Tanzania  huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi tarehe 8 June mwaka huu ambapo itakuwa ni miezi  miwili kabla ya uchaguzi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu