Mshauri wa zamani wa usalama wa Trump kuhukumiwa.

In Kimataifa

Mshauri wa zamani wa usalama wa taifa nchini Marekani Michael Flynn anatarajiwa kuhukumiwa leo katika mahakama kuu mjini Washington kwa kuwadanganya wachunguzi wa serikali. Mawakili wa Flynn, luteni jenerali mstaafu wa jeshi na mtu aliyekuwa karibu na Trump, ameomba asifungwe jela baada ya kukiri kuwa na hatia ya kuwadanganya maafisa wa shirika la FBI. Wameelezea ushirikiano aliotoa kwa maafisa katika uchunguzi kuhusiana na uingiliaji kati wa Urusi katika uchaguzi wa rais nchini Marekani mwaka 2016. Flynn alihojiwa mara 19 na kusaidia timu ya uchunguzi ikiongozwa na mwanasheria maalum Robert Mueller ambayo inaangalia uhusiano kati ya Urusi na kampeni ya rais Trump pamoja na kundi la maafisa wa kipindi cha mpito cha rais.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Majeshi ya Marekani yauwa raia Somalia

Majeshi ya Marekani yanayoendesha mashambulizi ya angani nchini Somalia dhidi ya ngome za wapiganaji wa Al Shabab nchini humo

Read More...

Idai yapoteza makazi ya watu 400,000.

Shirika la Msalaba Mwekundu linakadiria kuwa watu 400,000 wamepoteza makaazi yao nchini Msumbiji kutokana na Kimbunga Idai kilichoipiga nchi

Read More...

Baa la njaa kuikumba Kenya.

Zaidi ya watu milioni 1.5 nchini Kenya wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa kufuatia kutokuwepo kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu