Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, kwa tiketi ya CUF ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani ya chama chake kwa kile alichodai kuwa kumekuwa na migogoro ndani ya Chama chake, Mtolea ametoa tamko hilo ndani ya Bunge na kisha akatoka nje.
Uamuzi huo umekuja mara baada ya Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula kutangaza kufungwa kwa mlango wa Wabunge na Madiwani wanaotokea Upinzani jana mjini Morogoro na badala yake atakayetaka kujiunga na chama hicho baada ya hapo atakuwa mwanachama wa kawaida.