Rais Yoweri Museven wa Uganda amesema kuwa baadhi ya mawaziri wake si raia wa Uganda.
Museveni amemtaja waziri wa nchi anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Julius Wandera Maganda kuwa mmoja wa mawaziri ambao si raia wa Uganda.
Maganda na Aggrey Awori ambaye kutoka mwaka 2009 hadi 2011 alikuwa waziri wa Habari na Mawasiliano, wanatoka Busia, wilaya ya mpakani na Kenya na ni kilomita 196 mashariki mwa Kampala.
Museveni aliongeza kwamba wala hajui wanakotoka mawaziri wengine, kwa sababu kila anapowauliza huwa hawamwambii.
Alisema yote hayo kuonyesha mwingiliano wa kihistoria, utamaduni na lugha miongoni mwa watu wa nchi sita wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.