MVUA KUBWA YAHARIBU MAKAZI.

In Kitaifa

MVUA kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali, iliyonyesha katika kitongoji cha Makongeni katika kijiji cha Tairo Wilaya ya Bunda mkoani Mara, imesababisha kaya
5 kukosa makazi baada ya nyumba zake kuezuliwa na upepo huo na nyingine kubomoka.
ia mvua hiyo imeharibu mazao likiwemo zao la pamba, pamoja na mwanamke mmoja kujeruhiwa kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba na kulazwa hospitalini.
wenyekiti wa kitongoji hicho, John Bosco alitoa taarifa hiyo jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, aliyekuwa anafanya ukaguzi wa mashamba ya wakulima
a zao la pamba katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya mji wa Bunda.
osco alisema mvua hiyo ya mawe iliyoambatana na upepo mkali ilinyesha juzi kuanzia saa 11:00 jioni na kuleta uharibifu huo mkubwa. Alisema kwa sasa familia ambazo
yumba zao zimeezuliwa na nyingine kubomoka wanaishi kwa majirani na kwamba mwanamke aliyejeruhiwa hali yake inaendelea vizuri. Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti
uyo wa kitongoji aliiomba serikali kuwasaidia wahanga hao kwa namna moja ama nyingine. Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bupilipili, aliwapa pole waathirika hao akiwemo
wananchi mmoja ambaye shamba lake lenye ukubwa wa ekari mbili liliharibiwa na mvua hiyo.
liagiza halmashauri ya mji huo kupitia Idara ya Kilimo kumpatia mbegu nyingine mkulima huyo, ili aweze kupanda upya kwani msimu wa kilimo wa zao hilo bado
aujaisha. “Nawapa pole sana waathirika wote, Mkurugenzi hakikisheni mkulima huyu anapewa mbegu nyingine ili aweze kurudishia maana bado msimu wa kilimo wa zao
la pamba unaruhusu,” alisema. Akiwa katika kijiji cha Guta, Mkuu huyo wa Wilaya ya Bunda, pamoja na ujumbe wake alitembelea shamba la pamba la Shule ya Sekondari
uta na kuupongeza uongozi wa shule hiyo kutokana na kulima zao la pamba na shamba lao kuwa na ubora unaoridhisha.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu