MWAKINYO ASHUKURU

In Kitaifa

Bondia Hassan Mwakinyo, ametoa shukuran kwa watu
mbalimbali kwa ushirikiano ambao wamemuonesha katika
maandalizi ya pambano lake na Julius Indogo wa Namibia.


 Mwakinyo ametoa shukurani hizo kupitia ukurasa wake wa
Twitter ikiwa ni saa chache zimepita tangu, atetee ubingwa
wake wa Afrika (ABU) Super Welterweight baada ya kumpiga
Julius Indogo, raia wa Namibia raundi ya 4 kwa ‘TKO.’
 Pambano hilo limefanyika usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe
4 Septemba 2021, katika pambano lililofanyika ukumbi wa
Ubungo Plaza, Dar es Salaam.


 Mwakinyo ni bondia namba namba 1 Afrika na namba 37
duniani kati ya mabondia 2,050 wa uzani wa super welter.
Katika salamu zake, Mwakinyo amesema hivi;

Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu mana bila yeye
hakuna mimi, yeyee ndo mpangaji wa nani ashinde hakika
alinichagua mimi kuwa mshindi, pili nishukuru familia yangu
mama yangu bi Fatma Hassan na wengine wote kwa ujumla
ambao wamesimama na Mimi na kunitia nguvu pale kwenye
ugumu,


“Nishukuru management yangu kwa kazi kubwa walionayo juu
yangu,mkuu wangu wa mkoa,Serikali kuu, na wizara ya
michezo kwa ujumla kwa hakika najivunia,lakini pia sponsors,
(wadhamini) wote kama Azam na wengine wa pambano zima
toka mwanzo hadi mwisho lakini shukurani ya kipee ni kwako
shabiki wangu ambae ndani yako kuna mimi.
“Hakika ninyi mumenipa hadhi na heshima kubwa mimi sio
mshindi na nisingefika hapa bila ninyi, lakini kwa ambae pia sio
shabiki yangu nakushukuru sana bila kuwepo ninyi msiokuwa
mashabiki wangu nisingepata wa kunikosoa pale ninapokosea.
Nawashukuru sana. Ushindi huu ni wa Taifa zima…nitaendelea
kusimama kwa ajili ya nchi yangu…nawapenda sana…

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu