Mwakyembe aipongeza KMC

In Michezo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dokta Harrison Mwakyembe amepongeza mpango wa klabu ya KMC kujenga uwanja wake na kituo cha soka kwa vijana wadogo.

Akizungumza katika ziara fupi aliyofanya Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni ambayo inamiliki timu hiyo, Waziri Mwakyembe amesema kuwa KMC ni mfano wa kuigwa kwa mikakati wanayofanya.

Waziri mwakyembe amesema hatua waliyofikia uongozi wa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara haina budi kupongezwa na wizara yake, na ameahidi wizara hiyo kusaidia kwa chochote kile ambacho kitaonekana ni kufanyika.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu