Mwanafunzi afariki kwa kutoa Mimba.

In Kitaifa

Mwanafunzi Monica Ponera wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mtumbatimaji Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, amefariki baada ya kufanya jaribio la kutoa mimba ya Mapacha wawili kwa njia ya kienyeji.

Inadaiwa Mwanafunzi huyo alipelekwa kwa Mganga wa Jadi na Wazazi wake na kufanikiwa kumtoa mimba ya Mapacha wawili lakini afya yake ikawa mbaya kutokana na kupata maumivu makali, majeraha na upotevu wa damu nyingi, hata walipoamua kumpeleka Kituo cha Afya Namtumbo walishachelewa na licha ya Madakari kupambana kuokoa maisha ya Binti huyo ilishindikana.

Mwalimu Mkuu wa Mtumbatimaji Cuthbert Kilili anadai aliwapeleka Zahanati Wanafunzi 10 waliohisiwa kuwa na ujauzito na Mwanafunzi huyo (marehemu) pekee aligundulika kuwa na mimba ndipo Mwalimu akatoa taarifa Ofisi ya Mtendaji kwa hatua zaidi na inahisiwa kuwa ni chanzo cha Wazazi kuchukua uamuzi wa kwenda kumtoa mimba ili kukwepa mkono wa Sheria.

Mganga wa jadi anayetuhumiwa Isa Ligoma maarufu Mkweche amekana kuhusika na kusema Wazazi na Binti huyo walipita tu nyumbani kwake kupumzika kutokana na jua kali na safari ndefu wakieleka Kituo cha Afya Namtumbo, Mganga huyo na Wazazi wa Mtoto walifikishwa Kituo cha Polisi na kuhojiwa kisha kuachiwa kwa dhamana na upelelezi unaendelea.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu