Mwanamke Jifunze namna ya kujiongezea Thamani Katika Mahusiano yako.

In Mahusiano

Wadada wengi hudanganyika na kujiona wako na mwanaume sahihi eti kwa sababu
mwanaume huyo anampa pesa, anampeleka ku-enjoy maeneo ya gharama na
kadharika..hizo sio sifa pekee za mwanaume sahihi!
Hebu subiri kidogo, je mwanaume huyo amewahi kukuuliza kuhusiana na career na
ndoto zako?
Je matendo yake yana U-MUNGU ndani yake?, Je huwa anakuthamini muda wowote
na sio anapotaka sex pekee? Je amewahi kukushirikisha walahu robo tatu ya
vision(maono) yake na kuhitaji mawazo yako?
Je anakukumbuka kimawasiliano au inapita hata siku nzima hajawasiliana na
wewe?

Najua unaweza ukasema..”Ahhhh! sihitaji yote hayo” Mimi hapa nakwambia
unayahitaji sana hayo mambo niliyoeleza hapo juu kutoka kwa mwanaume
unayetaka kuwa na future nae.
Na unafahamu fika kwamba unayahitaji. Mwanaume sahihi kwako hataona taabu
kuyafanya hayo na zaidi kwako akiamini anakutengeneza kuwa malkia katika
paradiso yake,anajua utakuwa mbadala na msaada kwake na mama bora wa watoto
wake!
Huu ni muda wa kujiongezea thamani.
Hebu acha tabia ya kuwasifia wanaume wa kawaida kwa sababu ya vijizawadi vya
kupita na kuwaacha wale wenye kubeba ndoto na ubaadae wako kisa tu hawana pesa
za kukupa vitu bora na vya thamani kwa sasa, angalia ng’ambo ya mto unakotaka
kuvuka usiangalie hapo ufukweni uliposimama (mediocre men) !!!

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu