Mwanamke wa Indonesia anusurika kifungo jela kwa kuingiza mbwa msikitini

In Kimataifa

Mwanamke mwenye akili punguani amenusurika kifungo jela nchini Indonesia
kwa kukufuru baada ya kumbeba mbwa na kumuingiza msikitini.
Kanda ya video ya Suthe Margaret akiingia msikitini akiwa amevalia viatu
kabla ya kumruhusu mbwa wake ndani ya msikiti huo ilisambaa mwezi
Julai.


Ilizua hasira katika taifa hilo lenye Waislamu wengi ambapo mbwa
huonekana kuwa kitu kichafu.
Jopo la majaji mjini Bogor , mji uliopo karibu na mji wa Jakarta, lilimpata na
hatia ya kukufuru siku ya Jumatano lakini akasema kwamba hawezi
kuhukumiwa kwa kitendo chake.
Margaret anaugua ugonjwa wa paranoid schizophrenia, kulingana na
uchunguzi wa kiakili mwaka 2013.

Waendesha mashtaka wametaka apatiwe kifungo cha miezi minane jela.
Mwaamke huyo ambaye anaonekana kuwa na tatizo la kiakili anaingia
katika msikiti katika eneo la Bogor akisema kwamba yeye ni Mkatoliki na
kuongezea kwamba mumewe atafunga ndoa msikitini baadaye siku hiyo.
Anaushutumu msikiti kwa kumbadilisha dini huku mbwa huyo
akimzunguka.
Watu kutoka msikiti huo wanasema kwamba hawatambui harusi hiyo.
Mwanamke huyo baadaye anampiga teke bawabu wakati anapoambiwa
kuondoka.


Mbwa huyo baadaye anafariki baada ya kugongwa na gari

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TUME YA MADINI KWENYE MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI

Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akielezea fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini Tanzania katika

Read More...

Halmashauri ya Jiji la Arusha kutokomeza mimba za utotoni.

Halmashauri ya Jiji la Arusha ikishirikiana na wataalamu wa Afya kutoka mashirika mbalimbali, maafisa  elimu kata na sekondari,

Read More...

MNADA WA ALMASI WDL WAZIDI KUPAMBA MOTO.

Leo tarehe 20 Februari, 2020 mnada wa asilimia tano ya madini ya almasi kutoka katika Mgodi wa Williamson Diamond

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu