Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP) Kumpandisha Mahakamani IGP Sirro, DCI na AG

In Kitaifa
Mahakama Kuu nchini  imetoa wito wa kuwaita DCI, IGP na AG kufika mahakamani siku ya Jumatano ya tarehe 21 kujibu kesi ya kutomfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi  (TSNP) Abdul Nondo.
Taarifa za wito huo zimetolewa na Wakili wa Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Wakili Jebra Kambole.
Kambole amesema “Wito umetolewa  Mahakama kuu mbele ya Jaji Rehema Sameji. kwamba DCI, IGP na AG wanapaswa kufika mahakamani 21/03/2018 kujibu kesi ya Abdul Nondo”.
Kambole amesema washitakiwa katika kesi hiyo itakayosikilizwa Jumatano ni ; IGP  Sirro ambaye ameitwa kwasababu yeye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini hivyo vituo vyote na polisi wapo chini yake lakini bado Nondo amekuwa hapatikani katika vituo vya polisi.
Aidha Kambole amesema kuwa katika jalada lililofunguliwa, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), naye kahusishwa kwa sababu mara ya mwisho Nondo alipokelewa na yeye alipofikishwa Dar es salaam kutoka Iringa na kwamba alimchukua kama muathirika wa tukio la utekwaji na siyo mshtakiwa.
Hata hivyo Kambole amesema ameshafanya jitihada nyingi za kutaka kuonana na mteja wake lakini hadi sasa juhudi zake hazijafua dafu.
Abdul Nondo anashikiliwa na jeshi la polisi tanguMachi 7, ambapo awali aliripotiwa kupotea kusikojulikana na kesho yake kujikuta Iringa, ambapo Kamanda wa Polisi  Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa amesema mpaka sasa wanamshikilia Nondo kwa ajilili ya upelelezi na watakapokamilisha watamfikisha mahakamani.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu