Mwigulu Nchemba amezitaka jamii za kifugaji kuwapeleka watoto shule.

In Kitaifa

Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa jimboni la Iramba Magharibi, wa jamii ya kifugaji kuachana na  tamaduni za kutowapeleka watoto shule na kuwatumikisha kufuga mifugo yao.

Akizungumza wakati ziara yake jimboni Mwigulu amesema kuwa Urithi ulio mkubwa zaidi kwa mtoto ni Elimu,ambayo itamasaidia mtoto kwa maisha yake ya baadae.

Nchemba amezitaka jamii hizo kuachana na tamaduni ambazo zimepitwa na wakati kwani hali ya maisha imebadilika tofauti na miaka iliyopita.

Aidha amewataka kufuga kisasa kwa tija zaidi tofauti na hapo awali kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanasababisha ukame hivyo amewaasa kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto shule ili waje kuwa msaada kwa baadaye.

Hata hivyo, katika ziara yake hiyo ya jimboni kwake, Nchemba ametembelea ujenzi wa hosteli katika kila shule ya Sekondari katika Kata 20 na kujionea maendeleo ya ujenzi huo ambao unaendelea kwa kasi kubwa

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu