Mwili wa Rais wa zamani wa Marekani Bush kupewa heshima za mwisho.

In Kimataifa

Wabunge na wawakilishi wa bunge la seneti la Marekani wametoa heshima zao kwa rais wa zamani wa nchi hiyo George H.W Bush. Ikulu ya White House imewakilishwa na Makamu wa Rais Mike Pence aliyetoa shukrani kwa huduma ya uongozi aliyoitoa rais huyo wa 41 wa Marekani ambaye aliongoza kati ya mwaka 1989 hadi 1993. Pence amesema chini ya uongozi wa Bush Marekani iliweza kuvishinda Vita Baridi. Spika wa bunge Paul Ryan amesema mwendazake alikuwa mzalendo mkubwa. Mwili wa Busha utasalia huko Washington ambapo wananchi watakuwa na fursa ya kuuaga hadi kesho Jumatano. Hapo kesho itakuwa ni siku ya kitaifa ya maombolezo huko Marekani.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Kitambulisho cha Vladimir Putin cha ujasusi chapatikana Ujerumani.

Kitambulisho cha Vladimir Putin alichopewa kama jasusi Ujerumani alipokuwa anafanya kazi kama jasusi wa Urusi kimepatikana katika makavazi mjini

Read More...

May aairisha kura kuhusu Brexit.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameahirisha kura iliyokuwa ifanyike leo bungeni kuhusu makubaliano ambayo serikali yake na Umoja

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu