Mzozo umeibuka baina ya serikali ya Angola na upinzani juu ya mipango ya kuzika upya mwili wa aliyekuwa kiongozi wa vugugu la waasi wa Unita ambaye kifo chake kilitokea miaka 17 iliyopita na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa karibu miongo mitatu.
Serikali ilikuwa inataka kuukabidhi mwili wa Savimbi kwa wawakilishi wa Unita, ambacho sasa ni chama cha upinzani, ili waweze kuuzika mwili wake nyumbani kwao tarehe Mosi Juni.
Hata hivyo, makabidhiano ya mwili hayakufanyika na kila upande sasa unamlaumu mwingine.
Helena Savimbi, mmoja wa watoto wa kike wa kiongozi huyo wa waasi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba serikali haikuheshimu mkataba. “Ni mkanganyiko mkubwaIt’s ,” alinukuliwa akisema.
Serikali nayo imeishutumu Unita kwa kushindwa kuuchukua mwili Jumanne, kama walivyokubaliana.