Mzee Nulu awashangaza watu aongeza wake wanne, anaye watoto 100

In Kimataifa

Mzee Nulu Ssemakula anayetokea kijiji kiitwacho Ruyonza nchini Uganda amewashangaza watu kwa kuongeza wake wanne.

Hatua ya mzee huyo mwenye miaka 94 imekuwa ya kushangaza na kipekee katika kijiji hicho ambacho jamii yake imekuwa na ndoa ya mke zaidi ya mmoja,naye alikua akizingatia sana masuala ya familia na dini.

Alikuwa muislamu wa kwanza kutoka kujiji cha Ruyonza kwenda kuhiji Maka mwaka 1977, Gazeti la Daily Monitor la Uganda limeeleza.

Ssemakula anajivunia kuwa na wake 19 ambao amepata nao zaidi ya watoto 100, mdogo kabisa akiwa na umri wa miezi kumi na mke mdogo kabisa akiwa na miaka 24, ambaye ni mja mzito.
Hivi sasa anaishi na watoto wake wadogo 66.

Wakati baadhi ya watoto wake wana wajukuu, na mzee huyu anasema bado ana matumaini ya kuwa na watoto zaidi na hata wake wengi zaidi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mgombea urais wa chama tawala Burundi atangazwa mshindi kwa kupata asilimia 68.7

Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ametangazwa mshindi leo kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimedaiwa kukumbwa

Read More...

Watu 7 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi Wauawa Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi saba na kufanikiwa kukamata silaha ndogo Bastola

Read More...

Watanzania watakiwa kucheki afya zao na kufuata ushauri wa daktari.

Watanzania wametakiwa kuwa na mazoea ya kwenda vituo vya afya kucheki afya zao na kuacha dhana ya kutumia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu