Ndege mbili kupambana na nzige Longido

In Kitaifa

Serikali nchini imetangaza kuanza kutumia ndege kunyunyizia dawa makundi ya nzige yaliyovamia wilaya ya Longido na Simanjiro wakitokea nchini Kenya.

Taarifa za kuingia kwa wadudu hao waaribifu zilitolewa kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa na mkuu wa wilaya hiyo Frank Mwaibambe ambaye anasema ndege ya Shirika la Chakula Duniani FAO inayotokea Nairobi inatarajiwa kuanza kazi ya kunyunyuzia dawa leo.

Ndege ya serikali ya Tanzania nayo itaungana nayo mara tu rubani wake atakaporejea kutoka Ethiopia alikokwenda kusaidia kupambana na nzige pia.

Aidha mkuu huyo wa wilaya ameongeza kuwa mpaka sasa hakujawa na madhara yoyote kwani eneo lililovamiwa kwa kiasi kikubwa ni pori lakini pia asilimia kubwa ya nzige hao bado ni wadogo.

Mwaka jana makundi makubwa ya nzige yalivamia maeneo kadhaa nchini Kenya na Ethiopia na kuibua hofu ya kutokea kwa baa la njaa kutokana uharibifu mkubwa walioufanya.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wananchi Wa Siha Washukuru Serikali Kukabiliana na Nzige

Wananchi wa wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro wameipongeza serikali kwa hatua iliyochukua kudhibiti makundi ya nzige waliovamia maeneo

Read More...

JPM atoa mazito kwa Kijazi

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema alikosa mtu wa kumteua kuwa katibu mkuu kiongozi baada ya aliyekuwa akishika nafasi

Read More...

Wadukuzi wavamia tovuti za serikali ya Myanmar

Wahalifu wa kimtandao wamedukua tovuti za serikali inayodhibitiwa na jeshi nchini Myanmar hii leo, wakati kukiibuka mzozo wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu