Ndege sita kubwa za abiria zimetua kwenye uwanja wa ndege
wa kimataifa KIA ambapo hali hiyo inatajwa kueleta uwelekeo
mzuri katika sekta ya Anga ambayo imekuwa kwenye mdororo
kutokana na janga la Corona duniani.
Kaimu Mkurugenzi wa kiwanja cha ndege KIA Bi.Christine
Mwakatobe amesema ndege hizo zimewasili na watalii kutoka
mataifa mbalimbali na moja wapo imewasili kiwanjani hapo
ikiwa na abiria 180 wakiwemo mabilionea na wafanyabiashara
wakubwa.
