Ndege yatua kwa dharura kwenye shamba la mahindi…

In Kimataifa

Ndege ya abiria ya Urusi imelazimika kutua kwa dharura kwenye shamba la mahindi karibu na jiji la Moscow baada ya kugonga kundi la ndege.

Watu ishirikini na watatu wamejeruhiwa katika tukio hilo, ambalo limesababisha ndege kutua huku injini yake ikiwa imezima na gia yake ya kutua ikipata hitilafu.

Ndege hiyo Ural Airlines Airbus 321 ilikuwa ikisafiri kuelekea katika eneo la Simferopol Crimea ilipogonga kundi la ndege muda mfupi baada ya kuondoka uwanjani, hali iliyovuruga utendaji wa injini yake.

Vyombo vya habari vya taifa la Urusi vimetaja kutua kwa ndege hiyo kama muujiza wa eneo la Ramensk.

Maafisa wa ndege hiyo wamesema ndege imeharibika sana na haiwezi kupaa tena,na uchunguzi rasmi juu ya ajali hiyo unaendelea.

Ndege hiyo ilikwa na abiria 233 na wahudumu ndani yake, wakati ndege waliporipotiwa kuingia ndani ya injini na rubani wake akaamua kutua mara moja kwenye shamba la mahindi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mourinho kusuka kikosi chake.

Kocha mpya wa Tottenham Jose Mourinho atajaribu kumsajili tena mshambuliaji wa zamani wa Spurs Gareth Bale, 30, kutoka Real

Read More...

UNO ya Harmonize yawekwa private, Wasimamizi wa kazi zake waeleza.

Akizungumzia suala la kuripoti YouTube wimbo wa UNO, Magix amesema kuwa alimpa wiki moja Harmonize kumuomba msamaha kwa kutumia

Read More...

Bastola yadondoka na kuuwa mahakamani

Tukio la kusahangaza linalo Treand kwa sasa ni kuhusu kifo cha Mwendesha Mashitaka wa Serikali Afrika Kusini Addelaid Ferreira

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu