Ndugai Amtimua Bungeni Mbunge

In Kitaifa

Spika wa Bunge , Job Ndugai amemtimua bungeni mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvaa suruali inayombana.

Mbunge huyo wa Momba Condester Sichwale alitimuliwa bungeni na Spika, kulingana na kanuni za Bunge, ambazo zinawataka wabunge wanawake kutovaa suruali za kubana.

Hatua ya kufukuzwa bungeni kwa Mbunge Sichwale imekuja baada ya mbunge wa CCM wa Nyang’wale Hussein Amar kusimama na kuomba mwongozo wa Spika, huku akisema kuwa kuna wanawake waliokiuka kuvaa mavazi ya staha.

Spika Ndugai alimpa nafasi mbunge huyo kumtaja mwenzake aliyevaa mavazi ambayo hayakuwa na staha ili iwe mfano na ndipo alipoashiria alipokaa mbunge huyo bila kumtaja jina.

Hatahivyo Spika alisimama na kumtaka mbunge aliyevaa mavazi hayo asimame na aondoke ndani ya ukumbi ili akavae mavazi yenye staha ndipo atarejea tena bungeni.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SABAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake 5 wafikishwa mahakamani kwa makosa matano ikiwemo

Read More...

George Mkuchika Aaapishwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais Ikulu, Kazi Maalum.

Rais Samia Suluhu Hassan amemuapisha Kampeni Mstaafu George Mkuchika kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais Ikulu, Kazi Maalum. Kabla ya

Read More...

Al-Assad ashinda uchaguzi kwa asilimia 95 kura

Rais wa Syria Bashar al-Assad ameshinda muhula wa nne madarakani kwa kupata asilimia 95.1 ya kura zote zilizopigwa.

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu